Kuipenda Torati ya Mwenyezi Mungu
97 Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.
Ninaitafakari mchana kutwa.
98 Amri zako zimenipa hekima kuliko adui zangu,
kwa kuwa nimezishika daima.
99 Nina akili kuliko walimu wangu wote,
kwa kuwa ninatafakari kuhusu sheria zako.
100 Nina ufahamu kuliko wazee,
kwa kuwa ninayatii mausia yako.