Thawabu ya kumtii Mwenyezi Mungu
1 Heri wale wote wamchao Mwenyezi Mungu,
wanaoenda katika njia zake.
2 Utakula matunda ya kazi yako;
baraka na mafanikio vitakuwa vyako.
3 Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaao
ndani ya nyumba yako;
wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeituni
kuizunguka meza yako.
4 Hivyo ndivyo atakavyobarikiwa
mtu amchaye Mwenyezi Mungu.