9 Kumcha Mwenyezi Mungu ni utakatifu,
nako kwadumu milele.
Amri za Mwenyezi Mungu ni za hakika,
nazo zina haki.
10 Ni za thamani kuliko dhahabu,
kuliko dhahabu iliyo safi sana,
ni tamu kuliko asali,
kuliko asali kutoka sega.
11 Kwa hizo mtumishi wako anaonywa,
katika kuzishika kuna thawabu kubwa.