7 Kwa kuwa mfalme anamtumaini Mwenyezi Mungu;
kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.
8 Mkono wako utawashika adui zako wote,
mkono wako wa kuume utawakamata adui zako.
9 Wakati utajitokeza,
utawafanya kama tanuru la moto.
Katika ghadhabu yake Mwenyezi Mungu atawameza,
moto wake utawateketeza.