Sala ya asubuhi ya kuomba msaada
1 Ee Mwenyezi Mungu, tazama adui zangu walivyo wengi!
Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu!
2 Wengi wanasema juu yangu,
"Mungu hatamwokoa."
3 Lakini wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ni ngao yangu pande zote;
umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu.
4 Ninamlilia Mwenyezi Mungu kwa sauti kuu,
naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu.
5 Ninajilaza na kupata usingizi;
naamka tena, kwa maana Mwenyezi Mungu hunitegemeza.
6 Sitaogopa makumi elfu ya adui,
wanaojipanga dhidi yangu kila upande.