Maombi ya shukrani
1 Nitakutukuza wewe, Ee Mwenyezi Mungu,
kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,
na hukuacha adui zangu
washangilie juu yangu.
2 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nilikuita unisaidie
na wewe umeniponya.
3 Ee Mwenyezi Mungu, umenitoa Kuzimu30:3 Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, yaani Shimo lisilo na mwisho.,
umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.