Mwenyezi Mungu yuko pamoja nasi
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya wana wa Kora. Mtindo wa alamothi.
1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2 Kwa hiyo hatutaogopa, hata kama dunia ikiondolewa,
na milima ianguke kilindini cha bahari,
3 hata maji yake yakinguruma na kuumuka,
na milima itetemeke kwa mawimbi yake.