Kuomba msamaha
1 Ee Mungu, unihurumie,
kwa kadiri ya upendo wako usiokoma,
kwa kadiri ya huruma yako kuu,
uyafute makosa yangu.
2 Unioshe na uovu wangu wote
na unitakase dhambi yangu.
10 Ee Mungu, uniumbie moyo safi,
uifanye upya roho ya uthabiti ndani yangu.
17 Bali dhabihu za Mungu ni roho iliyovunjika;
moyo uliovunjika wenye toba,
ee Mungu, hutaudharau.