Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 86

Kuomba msaada

Maombi ya Daudi.

1 Ee Mwenyezi Mungu, sikia na unijibu,

kwa maana mimi ni maskini na mhitaji.

2 Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako,

wewe ni Mungu wangu,

mwokoe mtumishi wako anayekutumaini.

3 Ee Bwana, nihurumie mimi,

kwa maana ninakuita mchana kutwa.

4 Mpe mtumishi wako furaha,

kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana,

ninainua nafsi yangu.

5 Ee Bwana, wewe ni mwema na mwenye kusamehe,

umejaa upendo kwa wote wakuitao.

6 Ee Mwenyezi Mungu, sikia maombi yangu,

sikiliza kilio changu unihurumie.

7 Katika siku ya shida yangu nitakuita,

kwa maana wewe utanijibu.

8 Ee Bwana, katikati ya miungu hakuna kama wewe,

hakuna matendo ya kulinganishwa na yako.

9 Ee Bwana, mataifa yote uliyoyafanya

yatakuja na kuabudu mbele zako;

wataliletea utukufu jina lako.

10 Kwa maana wewe ni mkuu, na unafanya mambo ya ajabu;

wewe peke yako ndiwe Mungu.

11 Ee Mwenyezi Mungu, nifundishe njia yako,

nami nitaenda katika kweli yako;

nipe moyo usiositasita,

ili niweze kulicha jina lako.

12 Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nitakusifu kwa moyo wote;

nitaliadhimisha jina lako milele.

13 Kwa maana upendo wako ni mkuu kwangu;

umeniokoa kutoka vilindi vya kaburi86:13 Kaburi hapa ina maana ya Sheol kwa Kiebrania, yaani Kuzimu..

14 Ee Mungu, wenye majivuno wananishambulia;

kundi la watu wakatili linatafuta uhai wangu:

watu wasiokuheshimu wewe.

15 Lakini wewe, Ee Bwana, ni Mungu wa huruma na neema,

si mwepesi wa hasira,

bali ni mwingi wa upendo na uaminifu.

16 Nigeukie na unihurumie;

mpe mtumishi wako nguvu zako,

mwokoe mwana wa mjakazi wako86:16 au mwokoe mwanao mwaminifu.

17 Nipe ishara ya wema wako,

ili adui zangu waione nao waaibishwe,

kwa kuwa wewe, Ee Mwenyezi Mungu,

umenisaidia na kunifariji.

Veja também