Mwenyezi Mungu mlinzi wetu
1 Yeye akaaye mahali pa salama pake Yeye Aliye Juu Sana,
atadumu katika uvuli wake Mwenyezi.
2 Nitasema kumhusu Mwenyezi Mungu, "Yeye ndiye kimbilio langu na ngome yangu,
Mungu wangu, ninayemtumaini."
3 Hakika yeye ataniokoa na mtego wa mwindaji,
na maradhi ya kuambukiza ya kuua.
4 Atakufunika kwa manyoya yake,
chini ya mabawa yake utapata kimbilio,
uaminifu wake utakuwa ngao na kinga yako.