Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 92:12-15

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

12 Wenye haki watastawi kama mtende,

watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,

13 waliopandwa katika nyumba ya Mwenyezi Mungu,

watastawi katika nyua za Mungu wetu.

14 Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda,

watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,

15 wakitangaza, "Mwenyezi Mungu ni mkamilifu;

yeye ni Mwamba wangu,

na ndani yake hamna uovu."

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    12 Zab 52:8;Wim 7:7Mwenye haki atastawi kama mtende,

    Atakua kama mwerezi wa Lebanoni.

    13 Isa 60:21;Mt 15:13;Yn 15:2,5Waliopandwa katika nyumba ya BWANA

    Watastawi katika nyua za Mungu wetu.

    14 Watazaa matunda hadi wakati wa uzee,

    Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi.

    15 Kum 32:4;Rum 9:14Watangaze ya kuwa BWANA ni mwenye adili,

    Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    12 Wenye haki watastawi kama mtende,

    watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni,

    13 waliopandwa katika nyumba ya Bwana,

    watastawi katika nyua za Mungu wetu.

    14 Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda,

    watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu,

    15 wakitangaza, "Bwana ni mkamilifu;

    yeye ni Mwamba wangu,

    na ndani yake hamna uovu."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.