8 Mwenyezi Mungu ni mwenye neema na mwingi wa huruma,
si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo.
9 Mwenyezi Mungu ni mwema kwa wote,
ana huruma kwa vyote alivyovifanya.
10 Ee Mwenyezi Mungu, vyote ulivyovifanya vitakusifu,
watakatifu wako watakutukuza.
11 Watasimulia utukufu wa ufalme wako
na kusema kuhusu ukuu wako,
12 ili watu wote wajue matendo yako makuu
na utukufu wa fahari ya ufalme wako.