Mwito kwa ulimwengu kumsifu Mwenyezi Mungu
1 Msifuni Mwenyezi Mungu.148:1 kwa Kiebrania ni Hallelu Yah; pia 148:7, 14.
Msifuni Mwenyezi Mungu kutoka mbinguni,
msifuni juu vileleni.
2 Msifuni, enyi malaika wake wote,
msifuni yeye, enyi jeshi lake lote la mbinguni.
3 Msifuni yeye, enyi jua na mwezi,
msifuni yeye, enyi nyota zote zinazong’aa.