Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 19

Utukufu wa Mwenyezi Mungu katika uumbaji

1 Mbingu zinatangaza utukufu wa Mungu,

anga zahubiri kazi ya mikono yake.

2 Siku baada ya siku zinatoa habari,

usiku baada ya usiku zinatangaza maarifa.

3 Hakuna msemo wala lugha,

ambapo sauti zao hazisikiki.

4 Sauti yao imeenea duniani pote,

nayo maneno yao yameenea

hadi miisho ya ulimwengu.

Katika mbingu amepiga hema kwa ajili ya jua,

5 linafanana na bwana arusi

akitoka chumbani mwake,

kama shujaa anavyofurahia

kukamilisha kushindana kwake.

6 Huchomoza upande mmoja wa mbingu,

na kufanya mzunguko wake

hadi upande mwingine.

Hakuna kilichojificha joto lake.

7 Torati ya Mwenyezi Mungu ni kamilifu,

ikihuisha nafsi.

Shuhuda za Mwenyezi Mungu ni za kuaminika,

zikimpa mjinga hekima.

8 Maagizo ya Mwenyezi Mungu ni kamili,

nayo hufurahisha moyo.

Amri za Mwenyezi Mungu huangaza,

zatia nuru machoni.

Veja também