12 Alitenda miujiza machoni mwa baba zao,
huko Soani, katika nchi ya Misri.
13 Aliigawanya bahari akawapitisha,
alifanya maji yasimame imara kama ukuta.
14 Aliwaongoza kwa wingu mchana,
na kwa nuru ya moto usiku kucha.
15 Alipasua miamba jangwani
na akawapa maji tele kama bahari,
16 alitoa vijito kutoka jabali lililochongoka,
akayafanya maji yatiririke kama mito.