12 Mwa 32:3; Kut 7:8—12:32;Isa 19:11Mbele ya baba zao alifanya mambo ya ajabu,
Katika nchi ya Misri, konde la Soani.
13 Kut 14:21-22Aliipasua bahari akawavusha;
Aliyafanya maji yasimame kama ukuta.
14 Kut 13:21-22Akawaongoza kwa wingu mchana,
Na usiku kucha kwa nuru ya moto.
15 Kut 17:1-7;Hes 20:2-13;Zab 105:41;Isa 41:18Akapasua miamba jangwani;
Akawanywesha maji mengi kama maji ya vilindi.
16 Kum 9:21Akafanya vijito vitokeze katika mwamba,
Na kufanya maji yatiririke kama mito.