6 Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu,
nitegee sikio lako na usikie ombi langu.
7 Uoneshe ajabu ya upendo wako mkuu,
wewe unayeokoa kwa mkono wako wa kuume
wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.
8 Nilinde kama mboni ya jicho lako,
unifiche chini ya kivuli cha mabawa yako
9 kutokana na waovu wanaonishambulia,
kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.