Maombi ya mtu aliye uhamishoni
1 Kama ayala anavyoonea shauku vijito vya maji,
ndivyo nafsi yangu inavyokuonea shauku, Ee Mungu.
2 Nafsi yangu inamwonea Mungu kiu, Mungu aliye hai.
Ni lini nitaweza kwenda kukutana na Mungu?
3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu
usiku na mchana,
huku watu wakiniambia mchana kutwa,
"Yuko wapi Mungu wako?"
5 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?
Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?
Weka tumaini lako kwa Mungu,
kwa kuwa bado nitamsifu,
Mwokozi wangu na Mungu wangu.
11 Ee nafsi yangu, kwa nini unasononeka?
Kwa nini unafadhaika hivyo ndani yangu?
Weka tumaini lako kwa Mungu,
kwa kuwa bado nitamsifu,
Mwokozi wangu na Mungu wangu.