Hamu ya kusaidiwa na Mungu katika dhiki
1 Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji.
Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
2 Yn 7:37;1 The 1:9Nafsi yangu inamwonea kiu MUNGU, Mungu aliye hai,
Lini nitakapokuja nionekane mbele za Mungu?
3 Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku,
Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?
5 Zab 56:3,11;Isa 50:10;Omb 3:24Nafsi yangu, kwa nini kuinama,
Na kufadhaika ndani yangu?
Umtumainie Mungu;
Kwa maana nitakuja kumsifu,
Aliye afya ya uso wangu,
Na Mungu wangu.
11 Nafsi yangu, kwa nini kuinama,
Na kufadhaika ndani yangu?
Umtumaini Mungu;
Kwa maana nitakuja kumsifu,
Aliye afya ya uso wangu,
Na Mungu wangu.