Njia mbili
1 Mwa 5:24;Ayu 31:5;Zab 81:12;Mit 4:14Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
2 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.