Nchi zote zaitwa kumsifu Mungu
1 Mshangilieni BWANA, enyi nchi zote;
2 Mtumikieni BWANA kwa furaha;
Njoni mbele zake mkiimba;
3 Ayu 10:8,9;Mhu 12:1;Efe 2:10;Eze 34:30Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.
4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani;
Nyuani mwake kwa kusifu;
Mshukuruni, lihimidini jina lake;
5 1 Nya 16:34;2 Nya 5:13;7:3;Ezr 3:11;Zab 106:1;107:1;118:1;136:1;Yer 33:11Maana BWANA ni mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake katika vizazi vyote.