Ahadi ya mfalme juu ya uaminifu na haki
Ya Daudi. Zaburi.
1 Rehema na hukumu nitaziimba,
Ee BWANA, nitakuimbia zaburi.
2 1 Sam 18:14;Mwa 18:19;Kum 6:7;1 Fal 9:4 Nitakuwa na mwenendo usio na hatia;
Utakuja kwangu lini?
Nitakwenda kwa unyofu wa moyo
Ndani ya nyumba yangu.
3 Yos 23:6;1 Sam 12:20 Sitaweka mbele ya macho yangu
Neno la uovu.
Kazi yao waliopotoka naichukia,
Haitaambatana nami.
4 Mt 7:23;1 Kor 5:11;2 Tim 2:19 Moyo wa ukaidi utaondoka kwangu,
Lililo ovu sitalijua.
5 Mit 6:17;Lk 18:14 Amsingiziaye jirani yake kwa siri,
Huyo nitamwangamiza.
Mwenye macho ya kiburi na moyo wa majivuno,
Huyo sitamvumilia.
6 Rum 13:4 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,
Hao wakae nami.
Yeye aendaye katika njia kamilifu,
Ndiye atakayenitumikia.
7 Hatakaa ndani ya nyumba yangu
Mtu atendaye hila.
Asemaye uongo hatathibitika
Mbele ya macho yangu.
8 Yer 21:12;Hos 9:3 Kila asubuhi nitawaangamiza
Waovu wote nchini.
Nikiwatenga wote watendao uovu
Na mji wa BWANA.