Publicidade

Salmos 103

Shukrani kwa wema wa Mungu

Ya Daudi.

1 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Naam, vyote vilivyo ndani yangu

Vilihimidi jina lake takatifu.

2 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA,

Wala usizisahau fadhili zake zote.

3 Isa 33:24;Mt 9:2;Mk 2:5;Lk 7:47;Kut 15:26;Yer 17:14 Akusamehe maovu yako yote,

Akuponya magonjwa yako yote,

4 Aukomboa uhai wako kutoka kwa kaburi,

Akutia taji la fadhili na rehema,

5 Aushibisha mema uzee wako,

Ujana wako ukarejezwa kama tai;

6 BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki,

Na hukumu kwa wote wanaoonewa.

7 Alimjulisha Musa njia zake,

Wana wa Israeli matendo yake.

8 Kut 34:6;Hes 14:18;Kum 5:10;Yak 5:11 BWANA amejaa huruma na neema,

Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili.

9 Isa 57:16;Yer 3:5;Mik 7:18 Yeye hatashutumu daima,

Wala hatashika hasira yake milele.

10 Ezr 9:13 Hakututenda kulingana na hatia zetu,

Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu.

11 Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi,

Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao.

12 Isa 43:25;Efe 1:7 Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,

Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

13 Kum 8:5;Isa 63:15,16;Mal 3:17 Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake,

Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao.

14 Kwa maana Yeye anatujua umbo letu,

Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.

15 Mwanadamu siku zake zi kama majani;

Kama ua la kondeni ndivyo anavyostawi.

16 Maana upepo hupita juu yake, na kutoweka!

Lisionekane mahali lilipokuwa tena.

17 Kut 20:6 Bali fadhili za BWANA ni kwa wamchao

Tangu milele hata milele,

Na haki yake ni kwa vizazi vyote;

18 Kum 7:9 Kwa wale walishikao agano lake,

Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye.

19 Zab 47:2 BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbinguni,

Na ufalme wake unavitawala vitu vyote.

20 Mt 6:10 Mhimidini BWANA, enyi malaika zake,

Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake,

Mkiisikiliza sauti ya neno lake.

21 Mwa 32:2;Dan 7:9 Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote,

Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake.

22 Mhimidini BWANA, enyi matendo yake yote,

Mahali pote pa milki yake.

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-