Publicidade

Salmos 108

Sifa na sala ya ushindi

Wimbo. Zaburi ya Daudi.

1 Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,

Nitaimba, nitaimba zaburi,

Naam, kwa utukufu wangu.

2 Amka, kinanda na kinubi,

Nitaamka alfajiri.

3 Ee BWANA, nitakushukuru kati ya watu,

Nitakuimbia sifa kati ya mataifa.

4 Mik 7:18-20;Hes 14:18;Kum 7:9;Zab 36:5 Maana fadhili zako ni kubwa kuliko mbingu,

Na uaminifu wako unafika hata mawinguni.

5 Zab 57:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,

Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako.

6 Ili watu uwapendao waokolewe,

2 Unipe ushindi kwa mkono wako wa kulia, na uniitikie.

7 Mungu amenena kwa utakatifu wake,

Nami nitashangilia.

Nitaigawanya Shekemu,

Nitalipima bonde la Sukothi.

8 Mwa 49:10;Zab 60:7 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,

Na Efraimu ni nguvu ya kichwa changu.

Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,

9 Moabu ni bakuli langu la kunawia.

Nitamtupia Edomu kiatu changu,

Na kumpigia Filisti kelele za vita.

10 Zab 60:9 Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye boma?

Ni nani atakayeniongoza hadi Edomu?

11 Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa?

Wala, Ee Mungu, huendi na majeshi yetu?

12 Utuletee msaada juu ya mtesi,

Maana wokovu wa binadamu haufai.

13 Isa 25:10;30:3;Omb 1:15;Mal 4:3;Mdo 1:20;Ufu 14:19-20 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,

Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-