Publicidade

Salmos 126

Mavuno ya shangwe

Wimbo wa kupanda mlima.

1 Mdo 12:9 BWANA alipowarejesha mateka wa Sayuni,

Tulikuwa kama waotao ndoto.

2 Ayu 8:21 Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko,

Na ulimi wetu kelele za furaha.

Ndipo waliposema katika mataifa,

BWANA amewatendea mambo makuu.

3 BWANA alitutendea mambo makuu,

Tulikuwa tukifurahi.

4 Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa,

Kama vijito vya Kusini.

5 Isa 12:1-3;Yer 31:9;Yoe 2:17;Mt 5:4;2 Kor 7:8-11 Wapandao kwa machozi

Watavuna kwa kelele za furaha.

6 Ingawa mtu anakwenda zake akilia,

Azichukuapo mbegu za kupanda.

Hakika atarudi kwa kelele za furaha,

Aichukuapo miganda yake.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-