Nyumba ya mwumini yenye furaha
1 Heri kila mtu amchaye BWANA,
Aendaye katika njia yake.
2 Isa 3:10Taabu ya mikono yako hakika utaila;
Utakuwa heri, na kwako kwema.
3 Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,
Katika nyumba yako.
Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni
Wakiizunguka meza yako.
4 Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA.