Sala ya ukombozi kutoka kwa adui
1 Kum 31:17;Ayu 13:24;Zab 22:1;Isa 59:2Ee BWANA, utanisahau hadi lini, hata milele?
Hadi lini utanificha uso wako?
2 Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini,
Nikihuzunika moyoni mchana kutwa?
Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?