Publicidade

Salmos 136

Uumbaji wa Mungu na matukio ya kihistoria

1 1 Nya 16:34;2 Nya 5:13;7:3;Ezr 3:11;Zab 100:5;106:1;107:1;118:1;Yer 33:11 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

2 Kut 18:11;Kum 10:17 Mshukuruni Mungu wa miungu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

3 1 Tim 6:15;Ufu 17:14 Mshukuruni Bwana wa mabwana;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

4 Yeye peke yake afanya maajabu makuu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

5 Mwa 1:1;Mit 3:19 Yeye aliyeumba mbingu kwa fahamu zake;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

6 Mwa 1:2;Yer 10:12 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

7 Mwa 1:16;Kum 4:19 Yeye aliyeumba mianga mikubwa;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

8 Jua litawale mchana;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

9 Mwezi na nyota zitawale usiku;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

10 Kut 12:29 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wao wa kwanza;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

11 Kut 12:51 Akawatoa Waisraeli katikati yao;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

12 Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

13 Zab 78:13;Kut 14:21-29 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

14 Akawavusha Israeli katikati yake;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

15 Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

16 Kum 8:15 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

17 Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

18 Kum 29:7 Akawaua wafalme mashuhuri;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

19 Hes 21:21-30 Sihoni, mfalme wa Waamori;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

20 Hes 21:31-35 Na Ogu, mfalme wa Bashani;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

21 Yos 12:1 Akaitoa nchi yao iwe urithi;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

22 Urithi wa Israeli mtumishi wake;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

23 Mwa 8:1;Kum 32:36;Zab 102:17;Isa 63:9;Lk 1:48 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

24 Akatuokoa na watesi wetu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

25 Zab 104:27 Yeye akipaye kila kiumbe chakula chake;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

26 Mshukuruni Mungu wa mbingu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_12-11-46-