Publicidade

Salmos 144

Sala kwa ukombozi wa kitaifa na usalama

Ya Daudi.

1 2 Sam 22:35 Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu,

Aifundishaye mikono yangu vita,

Na vidole vyangu kupigana.

2 Mwamba144:2 Au Mhisani. wangu na ngome yangu,

Nguzo yangu na mwokozi wangu

Ngao yangu ninayemkimbilia,

Huwatiisha watu wangu chini yangu.

3 Ayu 7:17-18;Zab 8:4;Ebr 2:6 Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjali?

Na binadamu hata umwangalie?

4 Binadamu ni kama ubatili,

Siku zake ni kama kivuli kipitacho.

5 Isa 64:1 Ee BWANA, uziinamishe mbingu zako, ushuke chini.

Uiguse milima ili nayo itoe moshi.

6 Utupe umeme, uwatawanye,

Uipige mishale yako, uwafadhaishe.

7 Zab 69:1;Mal 2:11 Uinyoshe mikono yako toka juu, uniponye,

Unitoe katika maji mengi, kutoka kwa mkono wa wageni,

8 Vinywa vyao vinasema visivyofaa,

Na ambao mikono yao ya kulia ni ya uongo.

9 Zab 33:2 Ee Mungu, nitakuimbia wimbo mpya,

Kwa kinanda chenye nyuzi kumi nitakuimbia.

10 Awapaye wafalme wokovu,

Amwokoa Daudi, mtumishi wake, na upanga wa uovu.

11 Uniponye, unitoe,

Katika mkono wa wageni.

Vinywa vyao vyasema visivyofaa,

Na mkono wao wa kulia ni mkono wa uongo.

12 Wavulana wetu wakiwa ujanani wawe kama miche

Iliyostawi kikamilifu.

Binti zetu wawe kama nguzo za pembeni

Zilizochongwa144:12 au zilizonakishiwa. ili kupamba kasri.144:12 au hekalu.

13 Ghala zetu na zijae

Zenye akiba za jinsi zote.

Kondoo zetu na wazae

Elfu na makumi elfu mashambani mwetu.

14 Law 26:17 Ng’ombe wetu na wabebe mizigo mizito,

Kusiwe na kushambuliwa.

Wala kusiwe na kuhamishwa,

Wala malalamiko katika njia zetu.

15 Kum 33:29 Heri watu wenye hali hiyo,

Heri watu wenye BWANA kuwa Mungu wao.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-