11 Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kusena uweza wako.
12 Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
13 Ufalme wako ni ufalme wa milele,
BWANA ni mwaminifu katika maneno yake yote,
Na mwenye fadhili katika matendo yake yote145:13 Mistari hii miwili haiko katika makala ya Kiebrania, lakini iko katika makala ya Kigiriki iitwayo Septuaginta.
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote.