1 Haleluya.146:1 Haleluya: maana yake ni, Msifuni BWANA.
Ee nafsi yangu, umsifu BWANA.
2 Nitamsifu BWANA muda ninaoishi,
Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.
3 Isa 2:22 Msiwatumainie wakuu,
Wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.
4 Mhu 12:7;1 Kor 2:6 Pumzi yake inapomtoka, anarudi katika udongo wake,
Siku iyo hiyo mipango yake hutoweka.
5 Yer 17:7 Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,
Na tumaini lake ni kwa BWANA, Mungu wake,
6 Mik 7:20;Mdo 4:24;14:15;Ufu 14:7 Aliyezifanya mbingu na nchi,
Bahari na vitu vyote vilivyomo.
Huishika kweli milele,
7 Huwafanyia hukumu walioonewa,
Huwapa wenye njaa chakula;
BWANA hufungua waliofungwa;
8 BWANA huwafumbua macho waliopofuka;
BWANA huwainua walioinama;
BWANA huwapenda wenye haki;
9 BWANA huwahifadhi wageni;
Huwategemeza yatima na mjane;
Bali njia ya wasio haki huiharibu.
10 BWANA atamiliki milele,
Mungu wako, Ee Sayuni, kwa vizazi vyote.
Haleluya.