Sifa kwa wema wa Mungu kwa Israeli
1 Isa 42:10Haleluya.
Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.
3 Na walisifu jina lake kwa kucheza,
Kwa sauti tamu ya matari na kinubi.
4 Mit 11:20Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake,
Huwapamba wenye upole kwa wokovu.
5 Watauwa na waushangilie utukufu,
Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.