Publicidade

Salmos 149

Sifa kwa wema wa Mungu kwa Israeli

1 Isa 42:10 Haleluya.

Mwimbieni BWANA wimbo mpya,

Sifa zake katika kusanyiko la watauwa.

2 Ayu 35:10;Zek 9:9 Israeli na amfurahie Yeye aliyemwumba,

Wana wa Sayuni na wamshangilie mfalme wao.

3 Na walisifu jina lake kwa kucheza,

Kwa sauti tamu ya matari na kinubi.

4 Mit 11:20 Kwa kuwa BWANA awaridhia watu wake,

Huwapamba wenye upole kwa wokovu.

5 Watauwa na waushangilie utukufu,

Waimbe kwa sauti kuu vitandani mwao.

6 Kum 7:1-2;Ebr 4:12;Ufu 1:16 Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao,

Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.

7 Ili kufanya kisasi juu ya mataifa,

Na adhabu juu ya makabila ya watu.

8 Wawafunge wafalme wao kwa minyororo,

Na wakuu wao kwa pingu za chuma.

9 Kum 7:1-2;Ufu 5:10;Rum 16:20;1 Yoh 5:4 Kuwafanyia hukumu iliyoandikwa;

Hiyo ndiyo heshima ya watauwa wake wote.

Haleluya.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-