6 Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,
Utege sikio lako ulisikie neno langu.
7 Dhihirisha fadhili zako za ajabu
Wewe uwaokoaye wanaokukimbilia;
Kwa mkono wako wa kulia
Uwaokoe kutoka kwa adui zao.
8 Kum 32:10Unilinde kama mboni ya jicho,
Unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako;
9 Wasinione wasio haki wanaonionea,
Adui za roho yangu wanaonizunguka.