Shukrani za kifalme kwa ushindi
1 Kum 32:4;1 Sam 2:2;Zab 91:2Wewe, BWANA, nguvu yangu, nakupenda sana;
2 Ebr 2:13BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu,
Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia,
Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.
3 Zab 76:4Namwita BWANA astahiliye kusifiwa,
Hivyo nitaokoka na adui zangu.