Utukufu wa Mungu katika viumbe na hukumu
1 Isa 40:22;Rum 1:19Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu,
Na anga laitangaza kazi ya mikono yake.
2 Mchana husemezana na mchana,
Usiku hutolea usiku maarifa.
3 Hakuna usemi wala maneno,
Sauti yao haisikilikani.
4 Rum 10:18Sauti yao imeenea duniani kote,
Na maneno yao hadi miisho ya ulimwengu.
Katika hizo ameliwekea jua hema,
5 Mhu 11:7Nalo hutokeza kama bwana arusi akitoka chumbani mwake,
Lafurahi kama mtu aliye hodari
Kwenda mbio katika njia yake.
6 Mhu 1:5Kuchomoza kwake ni katika mwisho wa mbingu,
Na kuzunguka kwake ni hadi miisho ya mbingu,
Wala hakuna kitu
Kisichofikiwa na joto lake.
7 Sheria ya BWANA ni kamilifu,
Huiburudisha nafsi.
Ushuhuda wa BWANA ni amini,
Humtia hekima mtu asiye nayo.
8 Neh 9:13;Rum 7:12Maagizo ya BWANA ni ya adili,
Huufurahisha moyo.
Amri ya BWANA ni safi,
Huyatia macho nuru.