Sala ya ushindi
1 Isa 50:10BWANA akujibu siku ya dhiki,
Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.
2 Akutumie msaada toka patakatifu pake,
Na kukutegemeza toka Sayuni.
3 Azikumbuke sadaka zako zote,
Na kuzitakabali dhabihu zako.
4 1 Yoh 5:14,15Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako,
Na kukutimizia mipango yako yote.