16 Zek 12:10;Lk 23:33;Yn 20:27Kwa maana mbwa wamenizunguka;
Kusanyiko la waovu wamenisonga;
Wamenidunga mikono na miguu.
17 Naweza kuihesabu mifupa yangu yote;
Wao wananitazama na kunikodolea macho.
18 Mt 27:35;Mk 15:24;Lk 23:34;Yn 19:24Wanagawanya nguo zangu,
Na vazi langu wanalipigia kura.