Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 3

Mwamini Mungu katika dhiki

1 2 Sam 15:13—17:22BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,

Ni wengi wanaonishambulia,

2 2 Sam 16:8;Zab 22:7,8Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,

Hana wokovu huyu kwa Mungu.

3 2 Fal 25:27;Zab 27:6Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,

Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.

4 Kwa sauti yangu namwita BWANA

Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.

5 Zab 4:8;Mit 3:24;Mdo 12:6Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena,

Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.

6 Sitayaogopa maelfu na maelfu ya watu,

Waliojipanga Juu yangu pande zote.

Veja também