Publicidade

Salmos 3

Mwamini Mungu katika dhiki

Zaburi ya Daudi alipomkimbia mwanawe, Absalomu.

1 2 Sam 15:13—17:22 BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi,

Ni wengi wanaonishambulia,

2 2 Sam 16:8;Zab 22:7,8 Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu,

Hana wokovu huyu kwa Mungu.

3 2 Fal 25:27;Zab 27:6 Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote,

Utukufu wangu na mwinua kichwa changu.

4 Kwa sauti yangu namwita BWANA

Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu.

5 Zab 4:8;Mit 3:24;Mdo 12:6 Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena,

Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.

6 Sitayaogopa maelfu na maelfu ya watu,

Waliojipanga Juu yangu pande zote.

7 BWANA, uinuke, Mungu wangu, uniokoe,

Maana umewapiga taya adui zangu wote;

Umewavunja meno wasio haki.

8 Zab 37:39,40;Mit 21:31;Hes 13:4 Wokovu ni wa BWANA;

Baraka yako na iwe juu ya watu wako.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-