Zaburi. Wimbo wa kuweka wakfu hekalu. Ya Daudi.
1 Ee BWANA, nitakutukuza kwa maana umeniinua,
Wala hukuwafurahisha adui zangu juu yangu.
2 Zab 6:2-4 Ee BWANA, Mungu wangu,
Nilikulilia ukaniponya.
3 Zab 40:1,2 Umeniinua nafsi yangu,
Ee BWANA, kutoka kuzimu.
Umenihuisha na kunitoa
Miongoni mwao washukao Shimoni.
4 Mwimbieni BWANA zaburi,
Enyi watauwa wake.
Na kutoa shukrani.
Kwa kukumbuka utakatifu wake.
5 Zab 16:11;Ufu 22:17 Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu;
Radhi yake ni ya milele.
Kilio huweza kuwapo usiku,
Lakini furaha huja asubuhi.
6 Ayu 29:18 Nami nilipofanikiwa nilisema,
Sitaondoshwa milele.
7 Zab 104:29 BWANA, kwa radhi yako
Wewe uliuimarisha mlima wangu.
Uliuficha uso wako,
Nami nikafadhaika.
8 Ee BWANA, nilikulilia Wewe,
Naam, kwa BWANA niliomba dua.
9 Zab 115:17 Mna faida gani katika damu yangu
Nishukapo Shimoni?
Mavumbi yatakusifu?
Yatautangaza uaminifu wako?
10 Zab 4:1 Ee BWANA, usikie, unirehemu,
BWANA, uwe msaidizi wangu.
11 2 Sam 6:14 Umegeuza msiba wangu kuwa ngoma;
Umeniondolea huzuni yangu, kunijalia furaha tele.
12 Ili nafsi yangu ikusifu,
Wala isinyamaze.
Ee BWANA, Mungu wangu,
Nitakushukuru milele.