Ya Daudi. Funzo
1 Rum 4:7-8;Zab 85:2 Heri aliyesamehewa dhambi,
Na kuondolewa makosa yake.
2 Law 17:4;Rum 5:13;Yn 1:47;2 Kor 1:12 Heri ambaye BWANA hamhesabii hatia,
Na ambaye rohoni mwake hamna hila.
3 Nilipokosa kuungama dhambi zangu, mifupa yangu ilipooza
Kwa kulia kwangu mchana kutwa.
4 Kwa maana mchana na usiku
Mkono wako ulinilemea.
Jasho langu likakauka hata nikawa
Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.
5 Mit 28:13;Isa 65:24;Lk 15:18 Ndipo nikakuungamia dhambi yangu,
Wala sikuuficha upotovu wangu.
Nilisema, Nitayakiri maasi yangu kwa BWANA,
Nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu.
6 1 Tim 1:16;Isa 55:6;Yn 7:34 Kwa hiyo, hebu kila akuaminiye
Akuombe awapo katika dhiki.
Hakika maji makuu yafurikapo,
Hayatamfikia yeye.
7 Zab 9:9;Mit 18:10;Isa 4:6;Mt 23:37;Kol 3:3 Kimbilio langu utanilinda nisipate mateso,
Utanizungusha nyimbo za kufurahia wokovu wangu.
8 Isa 48:17 Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea;
Nitakushauri, jicho langu likikutazama.
9 Msiwe kama farasi wala nyumbu,
Wasiokuwa na akili.
Kwa matandiko ya lijamu na hatamu
Sharti kuwazuia hao, au hawatakukaribia.
10 Mit 13:21;Zab 34:8;Mit 16:20;Yer 17:7 Naye mtu mwovu ana mapigo mengi,
Bali amtumainiaye BWANA fadhili zitamzunguka.
11 Mfurahieni BWANA;
Shangilieni, enyi wenye haki
Pigeni vigelegele vya furaha;
Ninyi nyote mlio wanyofu wa moyo.