Uovu wa watu na wema wa Mungu
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi, mtumishi wa Bwana
1 Rum 3:18;Mwa 20:11;Mit 8:13;Mhu 12:3 Kuasi kwake yule mwovu hunena moyoni mwake,
Hakuna hofu ya Mungu mbele ya macho yake.
2 Kwa maana hujipendekeza machoni pake
Kuwa upotovu wake hautaonekana na kuchukiwa.
3 Yer 4:22 Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila,
Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.
4 Mik 2:1;Isa 65:2 Huwaza maovu kitandani pake,
Hujiweka katika njia mbaya; hauchukii ubaya.
5 Zab 57:10 Ee BWANA, fadhili zako zafika hata mbinguni,
Uaminifu wako hadi mawinguni.
6 Ayu 11:8;Rum 11:33;Ayu 7:20;Zab 145:9 Haki yako ni kama milima ya Mungu,
Hukumu zako ni vilindi vikuu,
Ee BWANA, unawalinda wanadamu na wanyama.
7 Rut 2:12 Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako!
Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
8 Ayu 20:17;Ufu 22:1 Watashibishwa kwa unono wa nyumba yako,
Nawe utawanywesha kutoka mto wa furaha zako.
9 Isa 12:3;Yer 2:13;Zek 13:1;Yn 4:10,14;Ufu 21:6;Mdo 26:18;Efe 5:8;Kol 1:13;1 Pet 2:9 Maana kwako Wewe iko chemchemi ya uzima,
Katika nuru yako tutaona nuru.
10 Yer 22:16 Uwadumishie wakujuao fadhili zako,
Na wanyofu wa moyo uaminifu wako.
11 Mguu wa kiburi usinikaribie,
Wala mkono wa wasio haki usinifukuze.
12 Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu;
Wameangushwa chini wasiweze kusimama.