Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 39

Sala ya kutaka hekima na msamaha

Kwa mwimbishaji: kwa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.

1 1 Fal 2:4;Mit 4:26,27;Ebr 2:1;Kol 4:5 Nilisema, Nitazitunza njia zangu

Nisije nikakosa kwa ulimi wangu;

Nitajitia lijamu kinywani,

Maadamu mtu mbaya awapo mbele yangu.

2 Nilikuwa sisemi, nilinyamaa kimya,

Sina faraja, maumivu yangu yakazidi.

3 Yer 20:9 Moyo wangu ukawa moto ndani yangu,

Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka;

Nilisema kwa ulimi wangu,

4 BWANA, unijulishe mwisho wangu,

Na idadi ya siku zangu ni ngapi;

Nijue jinsi maisha yangu yalivyo mafupi.

5 Zab 90:4 Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri;

Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako.

Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.

6 Kweli, watu wote hupita kama kivuli;

Wao hujisumbua bure tu;

Wanajirundikia mali wala hawajui ni nani atakayeirithi.

7 Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana?

Matumaini yangu ni kwako.

8 Uniokoe kutoka kwa maasi yangu yote,

Usinifanye niwe wa kulaumiwa na mpumbavu.

9 Nimenyamaza, sifumbui kinywa changu,

Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya.

10 Uniondolee pigo lako;

Kwa mapigo ya mkono wako nimeangamia.

11 Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake,

Watowesha uzuri wake kama nondo.

Kila mwanadamu ni ubatili.

12 Law 25:23;1 Nya 29:15 Ee BWANA, usikie maombi yangu,

Utege sikio lako niliapo,

Usiyapuuze machozi yangu.

Kwa maana mimi ni mgeni wako,

Msafiri kama baba zangu wote.

13 Ayu 10:20,21 Uache kunitazama, ndio nipate kufurahi tena,

Kabla sijafa na kutoweka kabisa.

Veja também