Publicidade

Salmos 4

Ombi la kuokolewa kutoka kwa adui

Kwa mwimbishaji: kwa ala za muziki zenye nyuzi. Zaburi ya Daudi.

1 Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo;

Uliniokoa nilipokuwa katika shida;

Unifadhili na kuisikia sala yangu.

2 Enyi wanadamu, hadi lini utukufu wangu utafedheheka?

Je! Mtapenda ubatili na kutafuta uongo hadi lini?

3 Kut 33:16;2 Pet 2:9 Bali jueni ya kuwa BWANA amejiteulia mtauwa;

BWANA husikia nimwitapo.

4 Efe 4:26;Mit 3:7 Muwe na hofu wala msitende dhambi,

Tafakarini vitandani mwenu na kutulia.

5 Kum 33:19;Zab 37:3 Toeni dhabihu za haki,

Na kumtumaini BWANA.

6 Zab 80:3 Wengi husema, Nani atakayetuonesha mema?

BWANA, utuinulie nuru ya uso wako.

7 Umenitia furaha moyoni mwangu,

Kupita yao wanapozidishiwa nafaka na divai.

8 Law 26:5;Kum 12:10;Yn 14:27;Flp 4:7 Katika amani nitajilaza na kupata usingizi mara,

Maana Wewe, BWANA, peke yako,

Ndiwe unijaliaye kukaa salama.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-