6 Zab 33:16Maana sitautumainia upinde wangu,
Wala upanga wangu hauwezi kuniokoa.
7 Bali Wewe ndiwe uliyetuokoa kutoka kwa watesi wetu;
Na watuchukiao umewaaibisha.
8 Zab 34:2;Rum 2:17;1 Kor 1:31Tumejisifia Mungu mchana kutwa,
Na jina lako tutalishukuru milele.