Ulinzi wa Mungu kwa mji na watu wake
Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Kwa mtindo wa Alamothi. Wimbo.
1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2 Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
3 Maji yake yajapovuma na kuumuka,
Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.