Ulinzi wa Mungu kwa mji na watu wake
Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Kwa mtindo wa Alamothi. Wimbo.
1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,
Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2 Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,
Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
3 Maji yake yajapovuma na kuumuka,
Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
4 Isa 8:7;Ufu 22:1;2 Nya 6:6;Zab 48:1;Isa 60:14;Ebr 12:22 Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu,
Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu.
5 Kum 23:14;Isa 12:6;Eze 43:7 Mungu yu katikati ya mji hautatetemeshwa;
Mungu atausaidia asubuhi na mapema.
6 Mataifa yanaghadhibika na falme kutetemeka;
Anatoa sauti yake, nchi inayeyuka.
7 BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
8 Njoni muyatazame matendo ya BWANA,
Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
9 Avikomesha vita hata mwisho wa dunia;
Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.
10 Kut 14:13;Isa 2:11 Tulieni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu,
Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.
11 BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,
Mungu wa Yakobo ni kimbilio46:11 Au ngome yetu. letu.