Publicidade

Salmos 47

Utawala wa Mungu juu ya mataifa

Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Zaburi.

1 Enyi watu wote, pigeni makofi,

Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe.

2 Kum 7:21;Neh 1:5;Mal 1:14 Kwa kuwa BWANA Aliye Juu, mwenye kuogofya,

Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote.

3 Zab 18:47 Amewatiisha watu wa nchi chini yetu,

Na mataifa chini ya miguu yetu.

4 1 Pet 1:4 Ametuchagulia urithi wetu,

Fahari ya Yakobo ampendaye.

5 Zab 24:7-10;Mdo 1:9;Efe 4:8-10;1 Tim 3:16 Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,

BWANA kwa sauti ya baragumu.

6 Mwimbieni Mungu sifa, imbeni sifa;

Imbeni sifa kwa mfalme wetu, imbeni sifa.

7 Zek 14:9;1 Kor 14:15 Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,

Imbeni kwa zaburi.

8 Mungu ayatawala mataifa,

Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.

9 Wakuu wa watu wamekusanyika,

Kama watu wa Mungu wa Abrahamu.

Maana ngao za dunia zina Mungu,

Ametukuka sana.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-