Wimbo. Zaburi ya Wakorahi.
1 Isa 2:2;Oba 1:17;Mik 4:1 Bwana ndiye aliye mkuu,
Na mwenye kusifiwa sana.
Katika mji wa Mungu wetu,
Katika mlima wake mtakatifu.
2 Mt 5:35;Yer 3:19;Omb 2:15;Eze 20:6;Isa 14:13 Kuinuka kwake ni mzuri sana,
Ni furaha ya dunia yote.
Mlima Sayuni, kule upande wa kaskazini,
Mji wa Mfalme mkuu.
3 Mungu katika majumba yake
Amejijulisha kuwa ngome.
4 2 Sam 10:6 Maana, tazama, wafalme walikusanyika;
Walikuja wote pamoja.
5 Mara Walipouona, wakashtuka;
Wakafadhaika na kukimbia.
6 Papo hapo tetemeko liliwashika,
Uchungu kama wa mwanamke azaaye.
7 Eze 27:26 Kama upepo wa mashariki
Unapovunja jahazi za Tarshishi.
8 Isa 2:2;Mik 4:1 Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona,
Katika mji wa BWANA wa majeshi.
Mji wa Mungu wetu;
Mungu atauimarisha hata milele.
9 Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu,
Katikati ya hekalu lako.
10 Mal 1:11 Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu,
Ndivyo na sifa yako hadi miisho ya dunia.
Mkono wako wa kulia umejaa haki;
11 Na ufurahi mlima Sayuni.
Binti za Yuda na washangilie
Kwa sababu ya hukumu zako.
12 Tembeeni katika Sayuni,
Uzungukeni mji wote,
Ihesabuni minara yake,
13 Tieni moyoni boma zake,
Yafikirini majumba yake,
Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja.
14 Isa 25:9 Kwa maana ndivyo alivyo
MUNGU, Mungu wetu.
Milele na milele
Yeye ndiye atakayetuongoza.